Jumamosi, 31 Machi 2018

KUKU WA SEKELA

 JINSI YA KUPIKA KUKU SEKELA (TANDOORI CHICKEN)

Mahitaji
Kuku vipande 6 visivyo na ngozi
Maziwa mrindi nusu kikombe
Paprika nusu kijiko cha chai
Coriander kijiko kimoja cha chai
Cayene pepper nusu kijiko cha chai
Cardamon robo kijiko cha chai
Karafuu iliyosagwa robo kijiko cha chai
Pilipili manga kijiko 1 cha chakula
Mafuta vijiko saba vya chakula
Garam masala kijiko kimoja

Maelekezo jinsi ya kupika
1.Chukua bakuli
2.Weka maziwa mgando (mtindi), limao, vitunguu saumu, tangawizi, jira, coriander, cayenne pepper, cardamon, karafuu, pilipili manga na chumvi.
3.Ukiona imechanganyika, ongeza garam masala, fenugreen na paprika endelea kuchanganya
4.Weka kuku ndani ya ule mchanganyiko, hakikisha ameenea viungo.
5.Ni vizuri ukimchana chana kuku kuruhusu viungo kuingia.Endelea kumgeuza kuku kwenye viungo mpaka uhakikishe kaenea kwenye viungo
6.Mtoe kuku nusu saa kabla ya kupika,mpake mafuta
7. Paka mafuta na kwenye chombo unachoenda kumpikia kuku
8.Panga kuku vizuri kwenye pan ya kuomea
9.Pik kwenye oven kwa dakika 35. Akiiva mtoe muanze kujiramba

KUKU YUPO TAYARI KWA KULIWA


PIA TUNAPOKEA OODA YA KUKU WA SEKELA KWA BEI NAFUU TU ZA MASHUGHULI
HAKIKA UNAPIKIWA KUKU NA KUHADITHIA WENGINE

TUTUMIE MESSAGE KWENYE UKURASA WETU Zanzibar Quality Bakery KWA MAHITAJI

KARIBUNI PIA KWA ODA ZA VYAKULA VYENGINE VINAPATIKANA KARIBUNI SANA







Jumatatu, 26 Machi 2018

Chapati laini


Unga wa ngano (wheat flour 1/2 of kilo)
Siagi vijiko 2 vya chakula
Yai (egg 1)
Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai)
Hiliki (ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
Maji ya uvuguvugu (warm water)
Mafuta (vegetable oil)


Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na  hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi ambayo imeyayushwa (Hakikisha iwe na umotoumoto)na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri.
Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge.
Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 15.
 Baada ya hapo tawanyisha unga katika madonge ya wastani (yasiwe makubwa sana au madogo sana) Ukimaliza hapo, andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao.
Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze. ukisha maliza ikunje (roll).
Fanya hivyo kwa madonge yote yaliyobakia.

Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani.
Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika) ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea.
Acha iive upande mmoja then igeuze upande wa pili. Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha. fanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue.
 ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyohiyvo mpaka chapati iive.
 Rudia hii process kwa chapati zote zilizobakia.


Siri ya chapati kuwa laini ni kutia siagi au mafuta ya kutosha kipindi unazikanda na pia kuzikanda mpaka unga uwe laini.



PIA TUNAPOKEA OODA YA CHAPATI KUANZIA HAMSINI
TUTUMIE MESSAGE KWENYE UKURASA WETU Zanzibar Quality bakery

Utaletewa mpaka ulipo Zanzibar

PIA ODA ZA VYAKULA VYENGINE VINAPATIKANA

Karibuni sana

Jumapili, 25 Machi 2018

Maandazi laini

 Katika muendelezo wa mapishi


Unga wa ngano (nusu kilo)
Sukari (Kikombe 1 cha ili hai)
Maziwa (kikombe1)
Maji ya uvuguvugu ya kukandia
Yai 1
Hiliki
Hamira kijiko kimoja cha chai
Tia unga kwenye bakuli kisha tia sukari,hamira, yai, maziwa  na hiliki kisha uchanganye pamoja mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia maji ya uvuguvugu kiasi na uanze kuukanda. Ni vizuri ukaukanda kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri.

Baada ya hapo Tawanyishaa unga uliokwandwa katika madonge 5. Tia unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati na hakikisha haiwi nyembamba sana wala nene sana yani inatakiwa iwe ya wastani.Ukishamaliza kusukuma unatakiwa ukate shape uipendayo na uyatandaze katika kitu kilichopo flat na kiwe kimenyunyuziwa unga wa ngano ili kuyazuia yasigandie. Rudia hiyo process kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo yaweke mandazi katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka (inaweza kuchukua saa 1 hadi mawili kuumuka). Yakisha umuka unatakiwa uweke mafuta katika karai la kuchomea. Hakikisha mafuta masafi ikiwezekana tumia mafuta ya sunflower ili kupata maandazi yanayopendeza.Yakisha pata joto la kiasi unatakiwa utumbukize mandazi na unaze kuyachoma mpaka yawe ya brown. Yakisha iva yaipue na uyaweke kwenye kitchen towel iliyakauke mafuta. Yakisha poa yatakuwa tayari kwa kuliwa.




Pia tunapokea oda ya maamaandazi ya harusi,chai 
Andazi moja ni shilling mia moja na hamsini(Oda ni kuanzia maandazi hamsini)

Pia tunapokea oda ya vyakula mbalimbali kuanzia hamsini 

Like page yetu ya facebook  Zanzibar Quality bakery ili kupata mapishi na oda 

Ijumaa, 23 Machi 2018

Oda oda oda



Je Nyumba yako haishi wageni????
Je unataka kunywa kahawa na vileja ???

Zanzibar Quality bakery ndio suluhisho

Kwa shilling elfu kumi na tano utapata vileja vya tende popote ulipo zanzibar
Vileja hivi ni kwa chakula cha nyumbani hata ofisini

Bila kusahau vyakula vingi vingi vinapikishwa kwa oda na hata kula mara moja

Fika Beit rass Bububu Zanzibar kwa kuweka oda

Au tutumie message kwenye ukurasa wetu wa Facebook
Zanzibar Quality bakery


Karibuni sana

Ijumaa, 9 Machi 2018

Oda oda oda

HABARI ZENU JAMANI

BEI ZA VYAKULA VYETU VYA ODA KUANZIA VYAKULA 50

Keki piece @ sh 500/-
Sambusa@sh 500/-
Vileja vya njugu @ sh 200/-
Vileja vya mchele @sh 150/-
Balfin @sh 250/-
Mkate wa ufuta @sh 500/-
Kachori @sh 150/-
Badia @sh 150/-
Katlesi @ sh 500/-
Eggchop@ sh 700 na 1200

BEI ZA VYAKULA VYA ODA KWA PIECE 1

Keki mayai 6 @sh 8000/-
Mkate wa mayai 6@sh 8000/-
Vileja vya mchele *120* sh 15000/-
Mkate wa mchele sh 8000/-
Vileja vya tende @sh 300/-
Vileja vya tambi @sh 250/-
Mabanzi sh 1000/-
Mikate mirefu 1500/-


KARIBUNI SANA
FIKA ZANZIBAR BEIT RASS MNARANI
AU WASILIANA NASI
0714648931 AU WHATSAPP 0714648931
FACEBOOK: Zanzibar Quality bakery
Au Tembelea www.zanzibarqualitybakery.blogspot.com

KARIBUNI SANA






KUKU WA SEKELA

 JINSI YA KUPIKA KUKU SEKELA (TANDOORI CHICKEN) Mahitaji Kuku vipande 6 visivyo na ngozi Maziwa mrindi nusu kikombe Paprika nusu k...