Jumapili, 25 Machi 2018

Maandazi laini

 Katika muendelezo wa mapishi


Unga wa ngano (nusu kilo)
Sukari (Kikombe 1 cha ili hai)
Maziwa (kikombe1)
Maji ya uvuguvugu ya kukandia
Yai 1
Hiliki
Hamira kijiko kimoja cha chai
Tia unga kwenye bakuli kisha tia sukari,hamira, yai, maziwa  na hiliki kisha uchanganye pamoja mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia maji ya uvuguvugu kiasi na uanze kuukanda. Ni vizuri ukaukanda kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri.

Baada ya hapo Tawanyishaa unga uliokwandwa katika madonge 5. Tia unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati na hakikisha haiwi nyembamba sana wala nene sana yani inatakiwa iwe ya wastani.Ukishamaliza kusukuma unatakiwa ukate shape uipendayo na uyatandaze katika kitu kilichopo flat na kiwe kimenyunyuziwa unga wa ngano ili kuyazuia yasigandie. Rudia hiyo process kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo yaweke mandazi katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka (inaweza kuchukua saa 1 hadi mawili kuumuka). Yakisha umuka unatakiwa uweke mafuta katika karai la kuchomea. Hakikisha mafuta masafi ikiwezekana tumia mafuta ya sunflower ili kupata maandazi yanayopendeza.Yakisha pata joto la kiasi unatakiwa utumbukize mandazi na unaze kuyachoma mpaka yawe ya brown. Yakisha iva yaipue na uyaweke kwenye kitchen towel iliyakauke mafuta. Yakisha poa yatakuwa tayari kwa kuliwa.




Pia tunapokea oda ya maamaandazi ya harusi,chai 
Andazi moja ni shilling mia moja na hamsini(Oda ni kuanzia maandazi hamsini)

Pia tunapokea oda ya vyakula mbalimbali kuanzia hamsini 

Like page yetu ya facebook  Zanzibar Quality bakery ili kupata mapishi na oda 

Hakuna maoni:

KUKU WA SEKELA

 JINSI YA KUPIKA KUKU SEKELA (TANDOORI CHICKEN) Mahitaji Kuku vipande 6 visivyo na ngozi Maziwa mrindi nusu kikombe Paprika nusu k...